Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe. Veronica Kessy amewaagiza Watendaji kata kuhakikisha wazazi na walezi wa wanafunzi wanapata chakula cha mchana shuleni.
Mhe. Kessy ametoa rai hiyo mapema leo wakati shule zinafunguliwa kwa muhula mpya wa masomo Januari 2025, huku akisisitiza kuwa wazazi wanaowajibu wa kusimamia wanafunzi wanapata chakula wakiwa shuleni kwa shule za Msingi na Sekondari.
Amesema hayo wakati wa Kikao cha Lishe kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa wilaya leo asubuhi Januari 13,2025 ambapo amewasisitiza watendaji wa Kata na Vijiji, wenyeviti wa Vijiji, Vitongoji kuhakikisha wanasimamia maadhimisho ya siku ya Lishe kwenye vijiji vyao bila kukosa na kuendelea kutoa elimu kwa kushirikiana na wataalamu wa Afya katika ngazi husika.
“Lishe ni Agenda ya Kitaifa hatutaki kusikia watoto wanapata utapiamlo wakati tunakila aina ya chakula kinachohitajika kwa watoto wetu, tuendelee kufanya mikutano ya kutoa elimu na kuhamasisha Jamii kutumia vyakula lishe na watoto waliopo shuleni kupata chakula siku zote za masomo” Alisema Mhe. Kessy
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa MbuluBi.Rehema Bwasi ameahidi Kuendelea kushirikiana na wataalamu ili kufatilia kwa undani suala la Lishe ili kutokomeza Kabisa udumavu na Ukondevu katika Halmashauri ya Mji wa Mbulu.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.