Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe. Veronica Kessy amewataka Wananchi wa Mbulu kupunguza ulevi huku watendaji wakitakiwa kuhakikisha wananchi wanafanya shughuli zinazowaingizia kipato
Mhe. Kessy amesema baadhi ya wananchi wamekuwa walevi kupindukia muda wa kazi na kushindwa kufanya shughuli za kiuchumi zinazoweza kuwaingizia kipato
Akizungunza kwenye kikao cha Kamati ya ushauri ya Wilaya leo Novemba 14,2024 amesema jamii inapaswa kufanya kazi kwa bidii na pombe zinywewe baada ya masaa ya kazi na kuwataka watendaji wa Kata kusimamia zoezi hilo.
“Baadhi ya wananchi hapa Mbulu Mjini na Mbulu Vijijini wanakunywa pombe kali hata ambazo zinawafanya walewe masaa ya kazi na hawawezi tena kufanya kazi, hakikisheni vilabu vya pombe vinafunguliwa baada ya muda wa kazi na kuwakamata wote wanaovunja sheria na wafikishwe kwenye mamlaka zinazohusika” Amesisitiza Mhe.Kessy
Sambamba na hayo amewasisitiza watendaji hao kuhakikisha mazingira yanakuwa safi katika maeneo yote ili kuweka Mitaa, Vitongoji na Vijiji safi na salama wakati wote ili kuepuka magonjwa ya mlipuko yanayoweza kuepukika.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.