CHMT MBULU MJINI WAMETAKIWA KUIMARISHA USHIRIKIANO ILI KUTOA HUDUMA BORA.
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu wa Mhe.Michael Semindu ameisisitiza timu ya Usimamizi wa Huduma za afya ya Halmashauri (CHMT) ya Halmashauri kuimarisha ushirikiano katika utendaji kazi ili kutoa huduma bora kwa wananchi.
Hayo yamesemwa leo Oktoba 9,2025 katika kikao kazi cha kilichokuwa na lengo la kujadili mwenendo mzima wa shughuli za idara ya Afya, Lishe na Ustawi wa jamii.
“Moja ya majukumu yenu ni kushirikiana kufanya kazi kwa bidii kwa maslahi mapana ya wilaya ya Mbulu kwani tupo kwa lengo moja tu kutoa huduma bora kwa Wananchi ili kuunga mkono jitihada za Serikali”alisema Mhe. Semindu
Awali akifungua kikao hicho Mhe. Semindu aliipongeza timu ya usimamizi wa huduma za afya kwa kutunukiwa Cheti cha Utoaji bora wa huduma na kupunguza vifo vya mama na mtoto.
Aidha, Mhe. Semindu amewakumbusha wataalamu kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika halmashauri hasa upande wa idara ya afya,lishe na Ustawi wa jamii
Nae Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)Ndugu.Lawarence Mlaponi amewasisitiza wataalamu wa afya kutokujihusisha na vitendo vya rushwa ili kuwahudumia wananchi katika haki na usawa.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.