Mradi wa kuboresha miji 45 nchini (TACTIC) umefika Halmashauri ya Mji wa Mbulu Mkoani Manyara kuangalia maeneo ambayo yanaweza kujengwa Stendi Kuu ya Mabasi, Soko na miundombinu ya Barabara.
Mradi huo unaoratibiwa na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupitia Wakala wa barabara za Mijini na Vijijini TARURA,huenda ukawa mkombozi kwa ujenzi wa miradi hiyo muhimu katika Halmashauri ya Mji wa Mbulu.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu Bi. Rehema Bwasi ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutupia jicho miradi muhimu katika kusogeza huduma karibu na wananchi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu Mhe. Peter Sulle amesema hii ni miradi iliyosubiriwa kwa muda mrefu na wananchi wa Mbulu na imekuwa kiu yao kubwa kuwa na Soko, Stendi ya Kisasa na hata barabara zinazopitika wakati wote.
Mradi huo wa TACTIC utatekelezwa katika Kata ya Imboru, Uhuru na Sanubaray.



Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.