Afisa Mwandikishaji Jimbo la Mbulu Mjini Bi. Anna P. Mbogo ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu, amefungua rasmi Mafunzo ya siku mbili (2) ya Uboreshaji wa daftari la wapiga kura Jimbo la Mbulu Mjini kwa Waandishi wasaidizi na BVR Operators leo tarehe 28.07.2019 katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Chief Sarwatt.
Zoezi hili la uandikishaji katika Jimbo la Mbulu Mjini litaanza tarehe 31.07.2019 hadi 06.08.2019 kwa kata zote 85 za Jimbo la uchaguzi Mbulu Mjini.
WALENGWA WA ZOEZI LA UANDIKISHAJI
Watanzania wote walioandikishwa kuwa Wapiga Kura hapo awali ambao wamehama Kata, waliopoteza au Kadi zao kuharibika, na wote wanaotaka kuboresha taarifa zao.
Watanzania wote wenye sifa za kuandikishwa kuwa Wapiga Kura na ambao kwa sababu moja au nyingine hawakuandikishwa hapo awali.
Watanzania watakaotimiza umri wa miaka 18 ifikapo siku ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020
Pia kuwaondoa wale ambao hawana sifa kama vile watu waliofariki.
AGIZO KWA WATAALAMU WANAOHUSIKA NA UBORESHAJI WA DAFTARI HILI.
Afisa Mwandikishaji Jimbo la Mbulu Mjini Bi. Anna P. Mbogo amewaasa kuheshimu sana masuala yote yanayohusu uchaguzi kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni za uchaguzi.
Amesisitiza wahusika wote wa zoezi la uandikishaji wapiga kura wafanye kazi kwa ushirikiano, bidii na weledi, pia kukaa katika kituo husika muda wote ili kufanikisha zoezi hili la uboreshaji wa daftari la wapiga kura.
Aliongeza kuwa wale ambao ni wazoefu basi wasifikiri wanajua kila kitu bali watumie fursa hii ya kuongeza ujuzi zaidi kisha wawe chachu ya utendaji kazi wenye matokeo chanya kwa Jimbo letu la Kiteto.
UHAMASISHAJI.
Kamati ya uhamasishaji zoezi hili litatoa matangazo kwenye mbao za matangazo, radio, na kutumia magari ya Matangazo yatakayopita kila mtaa/kijiji/kitongoji ili kuwasisitiza wananchi wajitokeze kwa wingi katika uborehsji huu. Suala la uhamasishaji ni la msingi na litafanywa katika Jimbo lote la Mbulu Mjini.
Aliongeza pia Wasimamizi wasaidizi ngazi ya Kata washiriki ipasavyo katika kuhamasisha na kutoa elimu kwa wananchi kwa kila kata ili kuwezesha zoezi hili lifanyike kwa ufanisi na weledi mkubwa.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.