Utaratibu wa kupata Leseni za Vileo
Sheria ya leseni za vileo imenyambulisha aina tisa za leseni za vileo zinazoweza kutolewa chini ya sheria hii: Retailers On Leseni hii humruhusu mwenye biashara kuuza pombe na kunywa eneo la biashara RETAILERS OFF Leseni hii haimruhusu mtu kinywea pombe eneo la biashara bali kwa watu wanaochukua kunyewea majumbani (Take away) kama Groceries. WHOLESALE Leseni hii ni kuuza pombe kwa jumla HOTEL Leseni hii humruhusu mwenye leseni kuuza pombe kwa ajili ya kunywea katika eneo la biashara kwa watu waliopanga hotelini kwa wakati wowote wa mchana na usiku RESTAURANT. Leseni hii inamruhusu mwenye leseni kuuza pombe kwa mtu yeyote anayekula chakula katika mgahawa katika muda wa saa 6.00 mchana hadi saa 8.00 mchana na saa 12.00 hadi saa 6.00 usiku.
MEMBERS CLUB Leseni hii huruhusu uuzaji wa pombe kwa kiasi chochote kwa mwanachama wa Klabu na wageni wao tu COMBINED Leseni ambazo zimeambatanishwa mbili kwa pamoja: (a) Combined Hotel and retailers on (b) Combined Hotel and Restaurant (c) Combined restaurant and retailers on TEMPORARY Leseni hii humruhusu mwenye leseni kuuza pombe katika sehemu iliyotajwa kwenye leseni mahali penye burudani, starehe au mkusanyiko mwingine kwa kipindi kisichozidi siku tatu LOCAL LIQUOR Class A Local Liquor Leseni hii humruhusu mwenye leseni kutengeneza pombe za kienyeji katika sehemu iliyotajwa na kuuza kwa ajili ya kunywea sehemu ya biashara au nje ya sehemu ya biashara.
Class B Local Liquor Leseni hii humruhusu kutengeneza pombe ya kienyeji sehemu iliyotajwa na kwenda kuuzia sehemu nyingine iliyo na leseni ya kuuza pombe za kienyeji Class C Local Liquor Leseni hii humruhusu kutengeneza pombe ya kienyeji katika sehemu iliyotajwa kwenye leseni na kuuza kwa mwenye class D au Class E Class D Local Liquor Leseni hii humruhusu kuuza pombe za kienyeji katika sehemu iliyotajwa kwenye leseni kwa kunywea eneo la biashara Class E Local Liquor Leseni hii humruhusu kuuza pombe za kienyeji kwa ajili ya kunyewea sehemu nyingine mbali ya eneo la biashara
1. MASHARTI YA KUPATA LESENI Mtu yeyote raia wa Tanzania anayo haki ya kupatiwa leseni ya Vileo ili mradi awe ametimiza umri wa miaka kumi na nane (18) mwenye akili timamu ambaye hajawahi kupatikana na kosa la jinai na awe na eneo la kufanyia biashara linalokubalika kisheria. Kwa mtu ambaye sio raia wa Tanzania anapaswa kuwa na kibali kinachomruhusu kufanya biashara nchini kutoka Idara ya Uhamiaji.
2. UTARATIBU WA KUPATA LESENI • Mwombaji hujaza fomu za maombi zinazotolewa na Manispaa • Eneo/jengo linalokusudiwa kufanyia biashara hiyo kukaguliwa na Afisa Afya, Afisa Mipangomiji, Polisi, Afisa Mtendaji wa Kata na Afisa Biashara wa Halmashauri na hutoa maoni yao kwenye fomu husika • Maombi hayo hupelekwa katika Malaka ya Utoaji wa Leseni za Vileo ya Wilaya kwa uamuzi • Mwombaji ambaye maombi yake yamepitishwa hupewa Leseni baada ya kulipa ada inayotakiwa na ni lazima amekamilisha masharti ya kupata leseni hapo juu.
VIWANGO VYA ADA Viwango vya ada vinavyotumika kwa sasa kwa aina mbalimbali za leseni ni kama zifuatavyo:- 1. Retailers On (Baa) - 30,000.00 hadi 40,000.00 2. Retailers Off (Grosari) - 20,000.00 hadi 30,000.00 3. Wholesale (Jumla) - 10,000.00 hadi 20,000.00 4. Members Club (Klabu Wanachama) - 10,000.00 hadi 20,000.00 5. Restaurant & Retailers On - 30,000.00 hadi 40,000.00 6. Temporary licence (Leseni ya muda) - 7,000.00 hadi 15,000.00 7. Hotel Licence (Leseni ya Hoteli) - 30,000.00 hadi 40,000.00 8. Retailers Off non-spirituous - 7,000.00 hadi 15,000.00 9. Retailers On – non-spirituous - 10,000.00 hadi 15,000.00 Mamlaka ya Vileo itaamua kiwango cha ada kitakachotozwa kati ya kiwango cha chini na kile cha kima cha juu. Viwango vinavyotumika kwa sasa na Halmashauri ni vile vya kima cha juu kwa kila aina ya leseni.
3. MASHARTI YA UTUMIAJI Leseni za vileo zina masharti mengi ikiwa ni pamoja na kutouza kilevi kwa watoto. Masharti mengine ni muda wa kuuza pombe na kelele za muziki. MUDA WA KUUZA POMBE BAA (RETAILERS ON) • Jumatatu hadi Ijumaa - Saa 12.00 jioni hadi saa 5.00 Usiku • Jumamosi, Jumapili na Sikukuu - Saa 5.00 asubuhi hadi saa 8.00 mchana na saa 12.00 jioni hadi saa 6.00 usiku GROSARI (RETAILERS OFF) • Jumatatu hadi Ijumaa - Saa 2.00 asubuhi hadi saa 1.00 jioni • Jumamosi, Jumapili na Sikukuu - Saa 3.00 asubuhi hadi saa 6.00 mchana RESTAURANT LICENCE (MGAHAWA) • Jumatatu hadi Ijumaa - Saa 6.00 mchana hadi saa 8.00 mchana na saa 12.00 jioni hasi saa 6.00 usiku • Jumamosi, Jumapili na Sikukuu - Saa 5.00 asubuhi hadi saa 8.00 mchana na saa 12.00 jioni hadi saa 6.00 usiku MAKOSA Baadhi ya makosa chini ya sheria hii: •
Kuruhusu biashara nyingine isiyokubalika kisheria kufanyika eneo la biashara • Kuuza pombe kwa mtu mwenye umri chini ya miaka kumi na sita (16) • Kuajiri mtu chini ya miaka kumi na sita (16) kuuza pombe • Kuruhusu mtu mwenye umri chini ya miaka kumi na sita kukaa eneo la kuuzia pombe • Kutoweka leseni sehemu ya wazi, ambapo itaonekana kwa urahisi na wakaguzi • Kumruhusu/kuleta fujo katika eneo la biashara • Kuruhusu eneo la biashara kutumika kama danguro • Kuuza pombe muda ambao ni kinyume cha sheria • Kufanya biashara ya pombe kwa kutumia leseni ya vileo ambao haistahili ADHABU Mfanyabiashara anayetenda mojawapo ya makosa haya akikamatwa, atafikishwa mahakamani na akitiwa hatiani atalipa faini au kifungo au adhabu zote kwa pamoja.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.