Saturday 21st, December 2024
@HALMASHAURI YA MJI WA MBULU
Mwenge wa uhuru uliwashwa kwa mara ya kwanza juu ya kilele cha mlima Kilimanjaro mwaka 1961. Mwenge huu unamulika ndani na nje ya mipaka ili kuleta matumaini pale ambapo kuna kukata tamaa, upendo pale kwenye chuki na heshima pale kwenye dharau. kila mwaka kuna mbio za mwenge zinazoanzia kwenye mikoa tofauti kuwakumbusha watanzania jukumu lao la kulinda umoja na amani ambavyo vimekuepo na kudumu. Halmashauri ya mji wa Mbulu umepokea Mwenge wa Uhuru tarehe 19/06 kata ya Tlawi, kitongoji cha Guneneda kutoka katika mikono ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu. Mwenge huo ukiongozwa na wakimbiza Mwenge sita (6), akiwemo;SAHILI NYANZABARA GERARUMA(NJOMBE), EMMANUEL NDEGE CHACHA(KAGERA), ZADIDA ABDALLAH RASHID(ZANZIBAR), RODRICK ROMWARD NDYAMUKAMA(MWANZA), ALI JUMA ALI na GLORIA FESTO PETER(SINGIDA). Halmashauri ya Mji wa Mbulu ulikimbiza mwenge Mwenge kilomita 113.3 na kuzindua miradi mitano ikiwemo barabara ya Lami(jiwe la msingi), mradi wa vijana(uzinduzi), tenki la maji,Qalieda(jiwe la msingi), madarasa mawili ya Nowu(uzinduzi) na kituo cha afya kainam( jiwe la msingi). Miradi hiyo imekuwa na thamani ya 1,686,780,737.86 fedha za kitanzania. Na kukabidhi Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Arusha tarehe 20/06.
Imeandaliwa na; Namnyack Mollel
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.