Ikiwa ni Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Watumishi wa Umma Leo 23/06/2025,Halmashauri ya Mji wa Mbulu imefanya kikao maalumu cha kusikiliza kero za Watumishi.
Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa Idara Ya Utumishi na Usimamizi 

wa Rasilimali watu Bi. Kulthum Seif amewaeleza Watumishi kuwa kuna umuhimu wa kujaza Taarifa katika Mfumo wa E- Utendaji.
“Sisi Watumishi tunapimwa utendaji kazi kwa kujaza taarifa zetu katika hivyo ni muhimu sana kuutumia mfumo wa E- utendaji kwa Wakati Sahihi ni kila siku”. Alisema Bi. Kulthum
Sambamba ya hayo Bi. Kulthum amewasisitiza Watumishi kufanya kazi kwa uzalendo ili kuiunga mkono Serikali na Kuzingatia sheria, kanuni na taratibu.
Maadhimisho ya wiki ya Watumishi wa Umma 2025 yamekuwa na Kaulimbiu isemayo “Himiza matumizi ya Mifumo ya Kidijiti ili kuongeza upatikanaji wa Taarifa na Kuchagiza Uwajibikaji”
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.