Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe.Zainab Katimba agosti23,2025 katika ufunguzi wa mashindano ya SHIMISEMITA 2025 katika Viwanja vya Mkwakwani Jijini Tanga.
Mhe. Katimba ameeleza kuwa uwepo wa bajeti ya kutosha utawawezesha Watumishi wengi kushiriki ipasavyo katika Mashindano ya SHIMISEMITA.
“Tunashiriki katika mashindano haya kwani huondoa msogo wa mawazo kwa watumishi,huwasaidia watumishi kubadilishana mawazo na lakini michezo hutela afya”.alisema Mhe.Katimba
Sambamba na hayo Mhe. Katimba amewasisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura ifikapo Oktoba 29 ili wachague Viongozi bora na waadilifu wanaowataka.
Sambamba na hilo amezitaka Halmashauri ambazo hazijashiriki kuleta wanamichezo kabla Mashindano hayajatamatika na kuwasihi watumishi kuendelea na mazoezi kwa ajili ya kujenga Afya.
Awali akitoa salamu za Mkoa wa Tanga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.Balozi Dkt. Batilda Buriani ameeleza kuwa jumla ya Halmashauri 150 zimeshiriki katika mashindano ya SHIMISEMITA 2025 yanayohusisha zaidi ya michezo 15 ikiwemo mpira wa Pete, soka na kikapu amesisitiza kuwa michezo imeleta chachu katika mzunguko wa Biashara Jiji la Tanga.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.