Maagizo hayo yametolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe. Michael Semindu katika kikao cha Robo ya Nne ya mwaka wa fedha 2024/2025 kilichoketi leo 19/08/2025 kwaajili ya kujadili na kufanya tathmini ya shughuli za lishe zilizofanyika kwa kipindi cha robo hiyo.
Mhe. Semindu amewaeleza Watendaji wa Kata kufanya ufuatiliaji kwa kushirikiana na Maafisa Lishe wa Halmashauri ili kujua usalama wa vyakula wanavyokula wanafunzi ikiwemo mazingira yanayotumiwa kupika vyakula na sehemu ambazo vyakula vinahifadhiwa.
“Ili tuwasaidie wanafunzi kuwa na afya njema na lishe bora, kila
mmoja wetu awe mstari wa mbele kufatilia maandalizi na uhifadhi wa vyakula vya wanafunzi mashuleni”, alisema Mhe. Semindu
Sambamba na hayo Mhe. Semindu amewasisitiza Watendaji kuendelea kusimamia na kuhakikisha siku ya lishe ya Kijiji inafanyika katika sehemu zao husika.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu, Bi. Rehema Bwasi ameahidi kuendelea kusimamia utekelezaji wa afua mbalimbali za lishe kwa kazi zote na amewaelekeza watendaji kutoa ushirikiano katika masuala mazima ya lishe.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.