Idadi ya wanafunzi wanaopatiwa huduma ya chakula katika Shule ya Msingi Waama imeongezeka kwa asilimia 83, kutoka wanafunzi 56 hadi 103 kuanzia darasa la 3 hadi la 7. Wanafunzi hao wanajumuisha wavulana (ME) 43 na wasichana (KE) 63.
Ongezeko hilo limetokana na Operesheni inayoendelea ya Watendaji wa Kata ya Uhuru katika Mitaa ya Buwa, Ayalabe, Maringo na Ayaraat, yenye lengo la kuhakikisha upatikanaji wa chakula shuleni na kuhamasisha wazazi kushiriki kikamilifu katika suala la lishe kwa watoto.
Kupitia operesheni hiyo, baadhi ya wazazi na walezi wameitikia mwito wa shule kwa kupeleka chakula kama walivyokubaliana, ikiwemo debe mbili za mahindi na kilo 15 za maharagwe kwa kila mwanafunzi.
Watendaji hao pia wamekagua ubora wa chakula kinachopikwa na kuliwa na wanafunzi na kubaini kuwa ni salama na bora kwa afya ya binadamu, tofauti na malalamiko yaliyokuwa yakitolewa awali na baadhi ya wazazi.
Takwimu zinaonyesha kuwa kufikia tarehe 21/08/2025 shule imepokea jumla ya magunia 30 ya mahindi, magunia 6 na debe 3 za maharagwe.
Msimamizi wa chakula shuleni hapo, Mwalimu Dorothea Gupchu, amesema kwamba ongezeko la wanafunzi wanaopata chakula limeonesha mwamko mkubwa wa wazazi na manufaa kwa watoto.
Hata hivyo, Mkuu wa Shule ya Msingi Waama, Mwalimu Tarsila John, amesema bado nguvu kubwa inahitajika ili wazazi wote wahamasike, kwani idadi ya wanafunzi wanaopata
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.