Mkuu wa Wilaya Ya Mbulu Mhe. Michael Semindu akiwa katika Ziara ya Ukaguzi wa Miradi amewakumbusha Wananchi juu ya Umuhimu wa Kulinda amani katika Maeneo wanayoishi.
“Kwa pamoja tuna jukumu la kulinda amani hivyo wananchi wote tuungane kupinga vitendo vyote vinavyo hatarisha maisha yetu”. Alisema Mhe. Semindu
Aidha, Mhe. Semindu amewasisitiza Wananchi kuendelea kushirikiana kuripoti matukio ya kikatili ili kuendelea kuhakikisha uwepo wa haki na usawa.
Sambamba na hayo Mhe.Semindu amewaeleza wananchi kuwa ni haki yao kupata huduma amesema Serikali inaleta fedha kwa lengo kuwasogezea huduma Wananchi.
Kwa niaba ya Wananchi wengine Bi. Juliana Paskali ameishukuru Serikali kwa Kuendelea kuwa karibu na Wananchi na kuendelea kutatua changamoto zinazowakabili.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.