Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu Bi.Rehema Bwasi wakati akifungua kikao kazi cha tathmini ya elimu cha mwezi kilicho wakutanisha Wakuu wa Shule za msingi zote za Halmashauri ya Mji wa Mbulu.
Bi.Rehema amaeeleza kuwa juhudi na usimamizi wa masuala ya elimu katika shughuli zetu zitaongeza kasi ya ufaulu kwa wanafunzi.
“Kuonekana kwa juhudi za utendaji kazi ni pale ambapo mwenendo wa taaluma za Wanafunzi unabadilika hasa kutoka kwenye hali hafifu Kwenda kwenye hali nzuri, Ushirikiano ni jambo pekee litakalo tufikisha katika mafanikio”.Alisema Bi.Rehema
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi Ndugu. Zakaria Nyinyimbe ameahidi kuendelea kushirikiana na walimu kulisukuma gurudumu la mafanikio,amewaeleza walimu kuendelea kufanya kazi kwa ukaribu na Ofisi ya Elimu Msingi.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.