Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendiga leo agosti5,2025 akizindua rasmi Maonesho ya nanenane ya 31 ya Kanda ya Kaskazini yanayofanyika Mkoa wa Arusha kwenye viwanja vya Themi- Njiro.
Mhe.Sendiga ameeleza kuwa lengo la nanenane ni kuonesha fursa zilizopo katika kilimo mifugo na uvuvi zinazochangia kuongezeka kwa pato la Taifa.
Aidha ameeleza kuwa Mpango wa Serikali ni kuhakikisha kilimo kinafanyika mwaka mzima tayari skimu mbalimbali za umwagiliaji zimeanzishwa katika maeneo tofauti Nchini.
Jumla ya Bilioni 139 zimetolewa kwa kanda ya Kaskazini katika Miradi ya umwagiliaji na ukarabati wa miundombinu.
"Mbolea za Ruzuku na mbegu za Ruzuku zimetolewa katika Uongozi wa Awamu ya Sita." Ameeleza Sendiga.
Sambamba na hayo amewataka Wataalamu kufanya tathimini ya kila mwaka ili kujua maendeleo ya wakulima na wafugaji pia kutathimini hali ya udumavu na utapia mlo.
Halmashauri ya Mji wa Mbulu ni miongoni mwa Halmashauri zinazoshiriki katika Maonesho ya nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Themi- Njiro Arusha kwa kanda ya Kaskazini.
Kauli mbiu ya Maonesho ya Nane nane 2025 inasema "Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo Mifugo na Uvuvi 2025".
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.