Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu aliyekuwa mgeni rasmi wakati akihutubia kwenye kilele cha Maonesho ya nanenane ya 31 Kanda ya Kaskazini yaliyofanyika viwanja vya Themi-Njiro Jijini Arusha.
Mhe. Babu ameeleza kuwa kampeni ya chanjo na utambuzi wa mifugo ni muhimu kwa kuwa itaenda sambamba na uboreshaji wa majosho, kujua idadi ya mifugo, kupunguza hatari za wizi wa mifugo na kuongeza thamani ya bidhaa za ngozi kwa kuacha alama za kimila kwenye mifugo.
“Kauli mbiu ya Maonesho haya ya nanenane imelenga kuhamasisha Wananchi kushiriki Uchaguzi Mkuu kwa Amani na utulivu”.ameeleza Mhe. Babu
Pia ameongeza kuwa siku mbili zimeongezwa ili kutoa fursa kwa Wananchi kuendelea kutembelea Mabanda na kuona teknolojia mpya na za kisasa zinazotumika katika uzalishaji wa bidhaa za kilimo,mifugo na uvuvi.
Awali akisoma taarifa ya Maonesho ya nanenane Katibu Tawala Mkoa wa Manyara Bi. Maryam Muhaji amesema kuwa jumla ya Taasisi 222 zimeshiriki katika Maonesho hayo na hadi kufikia Agosti 2025 jumla ya wananchi 35,984 wamehudhuria katika Maonesho hayo.
Kauli mbiu ya maonesho hayo mwaka huu 2025 ni “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025.”
Maonesho ya nanenane Kanda ya Kaskazini yatafungwa Agosti10, 2025.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.