Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe.Michael John Semindu Septemba15, 2025 alipofanya kikao na wafanyabiashara wote wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu kwa lengo la kusikiliza na kutoa majibu ya Serikali juu ya changamoto ambazo zimekua zikiwakabili wafanyabiashara hao.
Mhe. Semindu amewaeleza wafanyabiashara juu ya umuhimu wa kuwepo kwa ushirikiano kati ya wafanyabiashara na serikali ili pande zote mbili ziweze kufikia malengo.
“Serikali imelenga kuhakikisha kila mfanyabiashara anafikia malengo yake ya kibiashara,hivyo kila mfanyabiashara ana haki ya kuwasilisha changamoto ndiyo maana iko sababu ya kukaa na kujenga kitu kimoja kwa maendeleo ya Mbulu”, alisema Mhe.Semindu.
Kwa upande wake Meneja wa TRA wa Mbulu Mji Ndugu. Serapio Luanda amewaeleza wafanyabiashara juu ya umuhimu wa kutumia Dawati Maalumu la Uwezeshaji biashara ili kuiwezesha serikali kutambua biashara ya kila mwananchi.
Sambamba na hayo Ndugu. Luanda amewakumbusha wafanyabiashara kuendelea kulipa kodi kwasababu kodi ndiyo msingi wa maendeleo.
Kwaniaba ya wafanyabiashara wengine Ndugu.Saimon Bayo ameuomba uongozi wa Halmashauri kuwepo na maridhiano katika maamuzi ya ulipaji kodi.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.