Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendiga amewataka wananchi kutumia fursa ya Elimu ya Watu wazima ili kuepukana na utegemezi kwenye jamii.
Mhe. Sendiga ameyaeleza leo septemba04,2025 katika kilele cha maadhimisho ya juma la Elimu ya watu wazima yaliyofanyika kwa ngazi ya Mkoa katika stendi ya zamani Mjini Babati.
“Elimu ya Watu wazima inaendana na ujasiriamali hivyo twendeni tukawainge mkono wajasiriamali kwa kununua bidhaa zao ili kukuza uchumi wa Mkoa wa Manyara”. Alisema Mhe. Sendiga
Pia amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kuandaa mikakati inayotekelezeka ikiwa ni pamoja na kuandaa bajeti ili kufanikisha utekelezaji wa utoaji wa Elimu kwa Watu wazima.
Kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa wa Manyara Ndugu. Halfan Omary ameeleza kuwa Elimu ya Watu wazima ilianzishwa mnamo mwaka 1975 kwa Sheria ya Bunge namba 2.
“Takwimu ya sensa 2022 kwa Mkoa wa Manyara inakadiriwa kuwa asilimia 21.8 ya watu wazima wasiojua kusoma na kuandika”. Alieleza Ndugu. Halfan
Pia ameongeza kuwa Serikali ina mipango mbalimbali ya Elimu ya Watu wazima ikiwemo MEMKWA ,Mpango wa Elimu changamani vijana walio nje ya mfumo Rasmi( IPOSA),Mitihani Binafsi inayotolewa na NECTA.
Maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu wazima yalianza Septemba 02/2025 na kutamatika Septemba 4/2025.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.