Halmashauri zitakazopitiwa na Mwenge ikiwa ni pamoja na kukaguliwa na kuweka jiwe la msingi ni Halmashauri ya mji wa Mbulu,Mbulu Vijijini, Halmashauri ya Hanang, halmashauri ya Babati mji, Babati Vijijini, Halmashauri ya Simanjiro pamoja na kiteto.
Akipokea Mwenge wa uhuru kutoka mkoa wa Arusha mkuu wa mkoa wa manyara Alexander Mnyeti, alisema mwenge wa uhuru ni moja ya alama ya Uhuru umoja na utaifa wa watanzania hivyo kwa kuzingatia hilo wananchi wa Manyara wanatambua umuhimu wa mbio za mwenge wa uhuru kuwa ni chachu ya kuleta maendeleo na kuleta matumaini pale ambapo hapana matumaini upendo pale ambapo pana chuki na kuleta heshima sehemu palipojaa dharau.
Kati ya miradi 44 inayotarajiwa kuzinduliwa na mwenge wa uhuru ni pamoja na kuweka jiwe la msingi katika miradi 16 yenye thamani ya zaidi ya billion 3,kuzindua miradi 14 yenye thaman ya zaidi ya billion 2 pamoja nankuzindua miradi mbalimbali iliyogharimu zaidi ya million 600,kukagua miradi 10 iliyogharimu zaid ya billion 1 ambapo alieleza katika miradi hiyo nguvu za wananchi ni zaidi ya million 344 na serikali kuu ni jumla ya million 5899 na mamlaka za seikali za mitaa ni jumla ya million 211 na wahisani ni zaidi ya billion 1.
Aidha Mnyeti alisema wananchi wa mkoa wa manyara wameopokea vizuri mwenge wa uhuru na watatekeza kwa vitendo kauli mbiu yake inayoeleza kuwa "maji ni haki ya kila mtu tuunze vyanzo vyake na tukumbuke kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa"hakika ujumbe huo umesadifu na umelenga kuwafahamisha na kuwahamasisha wananchi kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji na kuwakumbusha kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa.
Ukiwa mkoani humo katika wilaya ya mbulu Mwenge ulifanikiwa kuzindua jumla miradi saba ambapo pia ulifanikiwa kuzindua mradi wa maji katika kata ya Barigish kijiji cha Arri Bans wenye thamani ya Tsh million 399 unaotarajia kuwakomboa na adha ya maji zaidi ya wakazi wapatao 4597 wa kata hiyo.
Akizungumza na wananchi wa mkoa wa manyara kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Mzee Mkongee Alli alisema kuwa ni takribani miaka 20 imefika toka kifo cha baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hivyo katika kimuenzi hatoacha kufanya kufanya kazi kwa bidii ikiwa ni pamoja na kupambana na adui Ujinga, Maradhi na Umasikini ikiwa ni pamoja kuwahamasisha wananchi kulipa kodi ili kuongeza pato la Taifa.
Aidha Mzee Mkongee alisema kuwa kwa kutambua umuhimu wa maji ilani ya Uchaguzi ya chama cha mapinduzi CCM ya mwaka 2015/2020 ni kuhakikisha ifikapo 2020 wananchi wote wanaoishi vijijini wanapata maji safi na salama kwa asilimia 85.
"Hivyo katika wa ilani hiyo kuanzia mwaka 2006 hadi mwaka 2018 kwa upande wa vijijini miradi ipatayo 1659 imeweza kukamilishwa kwa wakati lakini bado serikali inasera za kimkakati za uchimbaji wa visima vya maji virefu na vifupi ambavyo vimegharimu billion 14 " Alisema Mzee Mkongee.
Pia akawataka wananchi kutunza na kulinda vyanzo vya maji ili viweze kudumu kwa vizazi vya sasa na vizazi vijavyo ikiwa ni pamoja na kuacha kufanya shughuli za binadamu pembezo mwa vyanzo vya maji ikiwa ni kulima na kuchunga mifugo.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.