Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025,Ndugu Ismail Ally Ussi ameridhishwa na mradi wa jengo la mama na mtoto katika hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Mbulu ambalo limegharimu kiasi cha shilingi milioni 524.
Akizungumza mara baada ya kutembelea na kukagua jengo la mama Na mtoto Ndugu.Ussi amewasisitiza wananchi kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya sita kuwa kushiriki katika Shughuli za Maendeleo.
Sambamba na hayo Ndugu.Ussi amewasisitiza Wananchi kuendelea kulinda miundombinu ili kuweza kutumika kwa kizazi kijacho.
Aidha,Ndugu Ussi amepongeza uongozi wa Halmashauri kwa usimamizi wa Hospitali na kuwakumbusha Madaktari na wauguzi kutoa huduma bora ili kufikisha adhma ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa wananchi.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.