Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe.Michael Semindu leo 16/07/2025 amepokea Mwenge wa Uhuru 2025 kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe.Emmanuela Kaganda katika Uwanja wa Mpira wa Miguu Tsorii kata ya Gehandu.
Mwenge wa Uhuru 2025 katika Wilaya ya Mbulu utakimbizwa kwa siku Mbili katika Halmashauri ya Mji wa Mbulu na Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.
“Mwenge wa Uhuru Ukiwa Wilayani Mbulu utakimbizwa kilometa 196 na kuzindua, kuweka mawe ya Msingi na Kuzindua jumla ya miradi ya maendeleo yenye thamani ya Bilioni 44.3”. Alikiri Mhe.Semindu
Mwenge wa Uhuru 2025 katika Halmshauri ya Mji wa Mbulu utakimbizwa kilometa 92.5 na utatembelea ,kuzindua na kuweka Mawe ya Msingi jumla ya Miradi Nane (08) yenye thamani ya shilingi Bilioni 1.6.
Kauli mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 inasema “Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu”
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.