Afisa Mwandikishaji jimbo la Mbulu Mjini Bi. Rehema Bwasi leo Mei 14, 2025 amefungua mafunzo kwa waandikishaji wasaidizi na waendesha vifaa vya Bayometriki ngazi za Vituo, mafunzo yaliyoanza kufanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu.
Bi. Rehema akifungua mafunzo hayo amewasisitiza waandikishaji hao kuwa makini na waaminifu katika utendaji kazi wao wakati wote wa zoezi hili la uboreshaji wa Daftari la mpiga kura kwa awamu ya pili.
Sambamba na Mafunzo hayo Waandishi Wasaidizi na waendesha vifaa vya Bayometriki wamekula kiapo cha kutunza siri na kujivua uanachama.
Zoezi la uboreshaji wa Daftari hilo awamu ya pili linatarajiwa kuanza tarehe 16 Mei hadi 22 Mei, 2025 katika vituo vya Jimbo la Mbulu Mjini.
“Kujiandikisha kuwa Mpiga kura ni Msingi wa uchaguzi bora”





Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.