• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Barua pepe kwa wafanyakazi |
Halmashauri ya Mji Mbulu
Halmashauri ya Mji Mbulu

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Mbulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Biashara Viwanda na Uwekezaji
      • Mipango na Uratibu
      • Kilimo Mifugo na Uvuvi
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • UKAGUZI WA NDANI
      • USIMAMIZI WA MANUNUZI
      • FEDHA NA UHASIBU
      • MAWASILIANO SERIKALINI
      • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
      • HUDUMA ZA SHERIA
      • UHIFADHI WA MALIASILI NA MAZINGIRA
      • USIMAMIZI WA TAKA NA USAFI WA MAZINGIRA
  • Machapisho
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Kituo cha Habari
    • Press Release
    • Video
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Matukio
  • Miradi
    • Approved Project
    • Ongoing Project
    • Completed Project
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Huduma kwa watumishi
    • Maij
    • Elimu
    • Uvuvi
  • Kata
    • Ayamaami
    • Ayamohe
    • Bargish
    • Daudi
    • Endagikot
    • Gehandu
    • Gunyoda
    • Imboru
    • Kainam
    • Marangw
    • Murray
    • Nahasey
    • Nambis
    • Sanubaray
    • Silaloda
    • Tlawi
    • Uhuru
  • Uwekezaji
  • Madiwani
    • Peter Martin Sulle - Sanubaray
    • Alexander Amnaay Tango - Gehandu
    • Ally Akonaay Baha - Ayamohe
    • Anthon John Genda - Tlawi
    • Asia Shabani Amnaay - Bargish
    • Augustino Nade Panga - Nahasey
    • Basili Boay Gwawu - Imboru
    • Bayi Agustino Agapius - Endagikot
    • Emanuel Severino Malle - Kainam
    • Emanuel Akonaay Bura - Murray
    • Juliana Deengw Musso - Gunyoda
    • Kastuli John Umbe - Marang
    • Michael Safari Ami - Nambis
    • Mwajuma Athumani Kabuga - Uhuru
    • Peter Evaristi Golis - Daudi
    • Umbu Margwe Mayo - Ayamaami
    • Vita Kalamu Gilaksa - Silaloda
    • Anna Athanasi Hhayuma - Viti Maalum
    • Bernadetha Andrea Tsere - Viti Maalum

Wekahazina Wakalia Kuti Kavu, Ukusanyaji wa Mapato ya Ndani

Posted on: February 9th, 2020

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo ameagiza Wekahazina ambao Halmashauri zao hazifikia malengo waliyojiwekea kwenye ukusanyaji wa mapato ya ndani mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka huu wa Fedha watolewe  kwenye nafasi zao kwani watakua wameshindwa kutimiza jukumu lao la msingi lililopelekea kupewa cheo hicho.

Waziri Jafo ameyasema hayo leo alipokuwa akitoa taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya halmashauri kwa kipindi cha nusu mwaka (Julai – Disemba, 2019) kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

Jafo amesema Mamlaka ya Wekahazina iko chini yangu hivyo kwa yeyote atakayeshindwa kufikia malengo ya ukusanyaji atatupisha na watawekwa watu wengine wenye uwezo wa kufanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa na kufikia malengo tuliyojiwekea katika ukusanyaji wa mapato.

Halkadhalika aliongeza kuwa na Wakurugenzi wa halmashauri ambazo hazitafikia malengo atapeleka mapendekezo kwa Mamlaka inayohusika ili iweze kuwachukulia hatua stahiki kwa kushindwa kukusanya mapato inavyotakiwa na kurudisha nyuma jitihada za Serikali za kuongeza mapato.

Akizungumzia ukusanyaji wa Mapato hayo Waziri Jafo amesema kwa Mwaka wa Fedha 2019/20 Halmashauri zilipanga kukusanya Shilingi Bilioni 765.48 kutoka kwenye vyanzo vyake vya ndani na kipindi cha nusu mwaka (Julai hadi Desemba, 2019) Halmashauri zimekusanya Jumla ya Shilingi bilioni 356.81 ambayo ni asilimia 47 ya makisio ya mwaka.

Alifafanua kuwa taarifa za mapato ya vyanzo vya ndani katika kipindi cha Julai - Desemba, 2019 umeonesha kuwepo kwa ongezeko la mapato yaliyokusanywa kwa kiasi cha  Shilingi bilioni 56.7 ikilinganishwa na kiasi kilichokusanywa katika kipindi kama hicho cha Julai - Desemba, 2018 sawa na ongezeko la asilimia 19.

“Uchambuzi unaonesha kuwa Halmashauri 63 kati ya Halmashauri 185 zimekusanya mapato ya ndani kwa asilimia 50 na zaidi ya makisio kwa Mwaka wa Fedha 2019/20 na halmashauri mia ishirini na mbili (122) zimekusanya mapato ya ndani chini ya asilimia 50 ya makisio ya mwaka.

Aidha, Halmashauri hukusanya mapato mengi au kidogo kwenye vyanzo tofauti kulingana na hali halisi ya shughuli za kiuchumi za kila Halmashauri hivyo, ongezeko hilo limetokana na sababu mbalimbali ikiwemo ushuru wa zao la Korosho katika Halmashauri za Mikoa ya Mtwara na Lindi na Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma” alisema Jafo.

Aliongeza kuwa katika kipindi cha miezi sita (Julai – Desemba, 2019), Halmashauri za Wilaya za Tunduru na Kibondo zimekusanya mapato kwa asilimia 104 ya makisio ya mwaka 2019/2020.

Pia Waziri Jafo amezitaka Halmashauri zote zilizokusanya zaidi ya asilimia 100 hadi Desemba, 2019 na zile ambazo zimejitathmini na kuona upo uwezekano wa kuzidi asilimia 100 ya bajeti za mapato ya ndani ifikapo Juni, 2020 zinaelekezwa kufanya mapitio ya Bajeti kwa mujibu wa Sheria ya Bajeti ya mwaka 2015 ili ziweze kuongeza Bajeti za mapato na matumizi ya fedha hizo.

Jafo alisema katika kuzipima Halmashauri zote kwa kigezo cha wingi wa mapato (pato ghafi), Halmashauri ya Jiji la Dodoma imekusanya mapato mengi zaidi kuliko Halmashauri zote kwa kukusanya Shilingi Bilioni 29.75 na Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli imekusanya mapato kidogo kuliko Halmashauri zote kwa kukusanya Shilingi Milioni 186.10” Alisema Jafo.

Akifafanua Ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri Kimkoa kwa Kuzingatia Asilimia ya Makusanyo amesema Mkoa wa Geita umefanya vizuri ambapo umekusanya wastani wa asilimia 63 ya makisio ya Halmashauri za Mkoa huo.

Aidha, Mkoa wa mwisho kwa kigezo hicho ni Mkoa wa Tanga ambao umekusanya wastani wa asilimia 36 ya makisio ya mwaka ya Halmashauri za Mkoa huo.

Pia Waziri Jafo ameweka  wazi Ukusanyaji wa Mapato ya Ndani ya Halmashauri Kimkoa kwa Kuzingatia Wingi wa Mapato kuwa Mkoa wa Dar es Salaam umefanya vizuri kwa kukusanya kiasi cha Shilingi Bilioni 83.86 na  Mkoa wa mwisho katika wingi wa ukusanyaji wa mapato ni Mkoa wa Katavi ambao umekusanya Shilingi bilioni 4.68.

Akifafanua Ukusanyaji wa mapato kwa Halmashauri kwa Kuzingatia aina ya Halmashauri kwa Kigezo cha asilimia ya makusanyo ukilinganisha na makisio Waziri Jafo amesema kwa upande wa Majiji Jiji la Dar es Salaam limeongoza kundi la Halmashauri za Majiji kwa kukusanya mapato kwa asilimia 71 ya makisio yake na halmashauri ya Jiji la Dodoma imekuwa ya mwisho katika kundi hili ambapo imekusanya kwa asilimia 41 ya makisio yake ya mwaka.

Upande wa Manispaa, Ilemela imeongoza kundi hilo kwa kukusanya  asilimia 75 ya makisio yake na Manispaa ya Kigoma imekuwa ya mwisho ambapo imekusanya kwa asilimia 26 ya makisio yake.

“ Katika Halmashauri za Miji, Mji wa Njombe umeongoza kwa kukusanya kwa asilimia  88 ya makisio yake ambapo Halmashauri ya Mji wa Babati imekuwa ya mwisho kwa kukusanya asilimia 30 tu” alisema Jafo.

Aidha, kwa kundi la Halmashauri za Wilaya amesema  Wilaya za Tunduru na Kibondo zimeongoza kwa kukusanya asilimia 104 ya makisio ya mapato ya ndani kwa mwaka wa Fedha 2019/20 wakati Halmashauri za Mafia, Ukerewe na Gairo zimekuwa za mwisho katika kundi hilo kwa kukusanya asilimia 18 ya makisio.

Waziri Jafo aliongeza kuwa kwa upande wa mapato ya ndani ya Halmashauri kwa Kuzingatia Aina za Halmashauri kwa Kigezo cha Wingi wa Makusanyo Jiji la Dodoma limeongoza kwa kukusanya Shilingi bilioni 29.75 na Jiji la Dar es Salaam limekuwa la mwisho kwa kukusanya Shilingi bilioni 6.03.

“Halmashauri za Manispaa, Ilala imeongoza kwa kukusanya Shilingi bilioni 29.13 na  Manispaa ya Kigoma imekuwa ya mwisho katika kundi hili ambapo imekusanya Shilingi Milioni 694.93.

Halmashauri ya Mji wa Geita imeongoza kwa wingi wa mapato katika Halmashauri za Miji ambapo imekusanya Shilingi Bilioni 4.64. Halmashauri ya Mji wa Nanyamba imekuwa ya mwisho katika kundi hili ambapo imekusanya Shilingi Milioni 459.44” alisema Jafo.

Kwa upande wa Halmashauri za Wilaya, Chalinze imeongoza kwa kukusanya mapato mengi kwa Halmashauri za Wilaya ambapo imekusanya Shilingi Bilioni 3.89 na Wilaya ya Bumbuli imekuwa ya mwisho kwa kukusanya Shilingi Milioni 186.08.

Waziri Jafo alimalizia kwa kuzitaka Halmashauri zote kuendelea kukusanya mapato kwa njia ya kielektroniki na kudhibiti ukusanyaji wa fedha na mbichi na ameweka wazi kuwa     Taarifa ya mwisho ya kota ya nne ya ukusanyaji wa mapato ya ndani sambamba na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ataitoa tarehe 18.06.2020 kabla ya Bunge kuvunjwa hivyo kila mtu ahakikishe anatekeleza jukumu hili kwa ufanisi ili kufukia malengo.

Matangazo

  • TANGAZO LA HUDUMA ZA KIBINGWA KUANZA KUTOLEWA MBULU MJI May 26, 2025
  • KAMPENI YA UTOAJI WA MATONE YA VITAMINI A NA UPIMAJI WA HALI YA AFYA KWA MTOTO June 01, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA June 02, 2025
  • NJIA YA KUWASILISHA MALALAMIKO KUPITIA eMREJESHO December 16, 2024
  • Ona zote

Habari mpya

  • UMITASHUMTA NA UMISETA KURINDIMA IRINGA 2025

    June 02, 2025
  • WATUMISHI AJIRA MPYA MBULU TC WAPATIWA MAFUNZO YA PSSSF

    May 29, 2025
  • MBULU TC YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI

    May 28, 2025
  • MBULU MJI TUNAJIVUNIA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU-DT REHEMA BWASI

    May 27, 2025
  • Ona zote

Video

HOTUBA YA MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN BUNGENI
More Videos

Tovuti mashuhuri

  • Babati dc Website
  • Hanang' dc Website
  • Babati Town Website
  • Simanjiro Website
  • Kiteto Website
  • Mbuludc Website

Tovuti Mbadala

  • Manyara Reginal Website
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Ikulu
  • BLOG RASMI YA OFISI YA WAZIRI MKUU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali na Majibu
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.