• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Barua pepe kwa wafanyakazi |
Halmashauri ya Mji Mbulu
Halmashauri ya Mji Mbulu

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Mbulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Biashara Viwanda na Uwekezaji
      • Mipango na Uratibu
      • Kilimo Mifugo na Uvuvi
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • UKAGUZI WA NDANI
      • USIMAMIZI WA MANUNUZI
      • FEDHA NA UHASIBU
      • MAWASILIANO SERIKALINI
      • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
      • HUDUMA ZA SHERIA
      • UHIFADHI WA MALIASILI NA MAZINGIRA
      • USIMAMIZI WA TAKA NA USAFI WA MAZINGIRA
  • Machapisho
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Kituo cha Habari
    • Press Release
    • Video
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Matukio
  • Miradi
    • Approved Project
    • Ongoing Project
    • Completed Project
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Huduma kwa watumishi
    • Maij
    • Elimu
    • Uvuvi
  • Kata
    • Ayamaami
    • Ayamohe
    • Bargish
    • Daudi
    • Endagikot
    • Gehandu
    • Gunyoda
    • Imboru
    • Kainam
    • Marangw
    • Murray
    • Nahasey
    • Nambis
    • Sanubaray
    • Silaloda
    • Tlawi
    • Uhuru
  • Uwekezaji
  • Madiwani

Ugatuaji wa Madaraka ni muhimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa

Posted on: September 10th, 2019

Waziri Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amesema ili Mamlaka za Serikali za Mitaa ziweze kujiendesha lazima kuwepo na demokrasia  ambapo ugatuaji wa madaraka ni muhimu  katika  Mamlaka za Serikali za Mitaa

Ameyasema hayo leo wakati akifungua Kikao kazi  kati ya Menejimenti ya  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  na Watumishi kutoka Ofisi ya Rais Tawala na Serikali za Mitaa na Idara maalum ya Zanznibar  kilichofanyika katika  Ofisi za OR-TAMISEMI Jijini Dodoma.

Mhe. Jafo amesema katika kuhakikisha wananchi wanapata viongozi bora katika jamii Ofisi ya Rais TAMISEMI husimamia viongozi wa vijiji wasiopungua 12,000, viongozi wa Mitaa ambao wao wanapatikana katika Majiji, Manispaa na Halmashauri za Mijiambao ni zaidi ya 4000 na viongozi wa vitongoji zaidi ya elfu 64.

Amefafanua kuwa OR-TAMIEMI ni kiungo muhimu katika kusimamia utekelezaji wa sera mbalimbali zinazoandaliwa na Wizara zote nchini hivyo inaposhindwa kutimiza majukumu yake, kunakuwepo na ongezeko kubwa la Malalamiko kwa wananchi.

“Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ni kiungo muhimu katika Sekta zote ambapo isipotimiza wajibu wake kwa weledi haitatimiza lengo la Serikali la kuhakikisha uwepo wa maendeleo katika kila sekta nchini” Amefafanua Jafo.

Amesema kuwa OR-TAMISEMI ni watekelezaji wa Sera na miongozo mbalimbali inayotolewa na Wizara za Kisekta kwa kuwa ndio yenye Halmashauri ambazo hutoa huduma kuanzia ngazi ya kitongoji, kijiji na mtaa lengo likiwa ni kutatua kero mbalimbali za wananchi.

Amezitaja Taasisi ambazo zipo chini ya OR-TAMISEMI kuwa ni elimu Kibaha ambayo inasimamia masuala ya elimu, Taasisi ya Mabasi ya Mwendokasi, Chuo cha Hombolo ambacho kinaendesha mafunzo kwa ajili ya kutengeneza watumishi watakaosimamia utendaji kazi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa

Mhe. Jafo amesema ugatuaji wa madaraka hufanyika pia katika  Sekta ya Elimu ambapo  kazi ya Wizara ya Elimu ni kutunga Sera na miongozo mbalimbali wakati OR-TAMISEMI kazi yake ni  kusimamia miundombinu ya Elimu  kuanzia ngazi ya Msingi hadi Sekondari lengo likiwa ni kuboresha utoaji wa elimu nchini.

Hata hivyo amesema kwa upande wa Sekta ya Afya Serikali imeweza kufanya mabadiliko makubwa ambapo mpaka sasa Hospitali za Wilaya 67 zinajengwa na Vituo vya kutolea huduma 352 vimekarabatiwa na kujengwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini.

Amewataka watumishi kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Serikali za Mitaa na Idara maalum kutoka Zanzibar kujifunza kazi zinazofanywa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tanzania Bara ili waweze kufanyia kazi yale ambayo watayapata katika kikao kazi hicho.

Wakati huohuo Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Joseph Nyamhanga amewapongeza watumishi hao kwa kuamua kujifunza kuhusu ugatuaji wa madaraka katika Mamlaka za Serikali za Mitaa lengo likiwa ni kubadilishana uzoefu katika majukumu ili kuleta mabadiliko katika jamii.

Naye Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala na Serikali za Mitaa  na Idara Maalum  Zanzibar Mhe. Shamata Khamisi amesema kuwa lengo la ujio wao ni kubadilishana uzoefu kwa kuwa Zanzibar imeanza kupeleka majukumu kwa wananchi ikiwa ni ugatuaji wa madaraka.

Amesema kuwa kwa upande wa Zanzibar utekelezaji wa Sera ya ugatuaji wa madaraka inatakribani miaka miwili ambapo yapo mafanikio ambayo yanaonekana hivyo ni wajibu wetu kuja kujifunza zaidi  juu ya ugatuaji wa madaraka ili kuweza kuendelea  kutoa huduma bora kwa jamii.

 Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025 July 04, 2025
  • TANGAZO MUHIMU KUTOKA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI KUHUSU MAOMBI YA MPIGA KURA. September 15, 2025
  • TANGAZO LA HUDUMA ZA KIBINGWA KUANZA KUTOLEWA MBULU MJI May 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA MJI WA MBULU June 09, 2025
  • Ona zote

Habari mpya

  • TIMU YA WATAALAMU(CMT) YAFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA MIRADI

    October 18, 2025
  • WATANZANIA WAMETAKIWA KUILINDA AMANI

    October 14, 2025
  • HATI MILIKI 48 ZA ARDHI ZATOLEWA KWA WANANCHI MBULU MJINI.

    October 09, 2025
  • CHMT MBULU WAMETAKIWA KUIMARISHA USHIRIKIANO ILI KUTOA HUDUMA BORA.

    October 09, 2025
  • Ona zote

Video

HOTUBA YA MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN BUNGENI
More Videos

Tovuti mashuhuri

  • Babati dc Website
  • Hanang' dc Website
  • Babati Town Website
  • Simanjiro Website
  • Kiteto Website
  • Mbuludc Website

Tovuti Mbadala

  • Tamisemi
  • Ikulu
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • Mbulu Tc Facebook
  • Mbulu Town Council WatsApp
  • Mbulu Tc Instagram

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali na Majibu
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.