Wananchi Wilayani Mbulu Mkoani Manyara wametakiwa kuwa mabalozi katika mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi.
Rai hiyo imetolewa mapema leo Disemba 1, 2024 na Mbunge wa Jimbo la Mbulu Mjini Mhe. Zakaria Isaay akiwa mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani yaliyofanyika katika kijiji cha Kwermus Kata ya Nambis Halmashauri ya mji wa Mbulu ambapo amewasihi wananchi kuacha tabia ya kujihusisha na ngono zembe.
"Tukiwa tunaadhimisha siku hii muhimu, niwasihi tu wananchi wa Mbulu kuwa ni vema kila mmoja wetu kutambua umuhimu wa kupambana na maambukizi mapya ya VVU ili kulinda Jamii yetu ya sasa na baadaye".
Maadhimisho hayo yamefanyika leo yakiwa na kauli mbiu isemayo "Chagua njia sahihi kutokomeza UKIMWI"
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.