Timu ya Wataalamu wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu imetembelea kuona utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa Katika Halmashauri.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Mbulu Ndugu Ally Msangi amewakumbusha Wataalumu Kuendelea kushirikiana katika Utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili iweze kuanza kutumika kwa wakati.
Aidha, ameongeza kwa kuwasisitiza wasimamizi wa miradi kuwashirikisha wataalamu wote changamoto ambazo zinajitokeza wakati wa utekelezaji wa miradi ili ziweze kufanyiwa kazi na kutatuliwa haraka.
Sambamba na hayo wajumbe wamesisitiza kufuata utaratibu katika hatua za manunuzi katika vifaa vya ujenzi.
Miradi iliyotembelewa ni Jengo la Utawala lenye thamani ya Bilioni 3.4 linalojengwa katika Kata ya Sanubaray na nyumba ya Mkurugenzi yenye thamani ya Milioni 150 inayojengwa Katika Kata ya Sanubaray.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.