Halmashauri ya Mji wa Mbulu Mkoani Manyara imedhamiria kuhakikisha wazee wasiojiweza wanapata Vitambulisho vya msamaha ili waweze kupata matibabu bure Hospitalini.
Hayo yamesema na Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya Mji wa Mbulu Ndg. Tomic Simbeye wakati akizingumza na Wazee wa Kata ya Endagikot na Sabubaray leo tarehe 12 Novemba, 2024.
Simbeye amesema “Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejipanga vema kutoa huduma za afya zenye ubora na gharama nafuu ambapo kwa upande wa wazee wasiojiweza wameanza kuandikishwa ili wapewe Vitambulisho”.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.