Kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Tarehe 27/11/2024,Kamati ya Rufaa ya Wilaya ya Mbulu imepewa Mafunzo maalumu ili kuhakikisha uchaguzi wa serikali za Mitaa unafanyika kwa kuzingatia Haki na Usawa.
Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi Halmashauri ya Mji wa Mbulu Bi. Rehema Bwasi akizungumza na Kamati ya rufaa ya Wilaya ya Mbulu amewakumbusha kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, kanununi na taratibu ili kuhakikisha uchaguzi wa Serikali za Mitaa unafanyika kwa kuzingatia haki na usawa.
“Nendeni mkafanye kazi kwa uaminifu na kuzingatia 4R za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku wote tukionyesha ushirikiano wa hali ya juu".Alisema Bi.Rehema
Sambamba na mafunzo hayo Hakimu Mkazi Mwandamizi Wilaya ya Mbulu Mhe. Vitus Eusebius Kapugi ameiapisha kamati ya rufaa iiapo cha uadilifu na kiapo cha kutunza siri.
"Serikali za Mitaa Sauti ya wananchi Jitokeze kushiriki uchaguzi"
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.