Rais Magufuli, ametangaza kuwa kuanzia June Mosi, 2020 vyuo pamoja na kidato cha sita vitafunguliwa kuendelea na masomo.
Amesema kuwa vyuo vyote vifunguliwe tarehe moja June na kuitaka Wizara ya Elimu na Wizara ya Fedha kuandaa utaratibu mzuri wa wanafunzi kupata mikopo watakapofika vyuoni na kuhusu wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari, utaratibu utatolewa hapo baadaye.
“Tumeamua sisi kama Serikali vyuo vyote vifunguliwa tarehe moja Juni, 2020. Niwaombe sana wizara zinahohusika hasa Wizara ya Elimu na Wizara ya Fedha ambayo inahusika katika kutoa mikopo, ina siku 9 zijiandae ili vyuo vitakapofunguliwa kusiwe na kero zingine“ JPM
“Ukianchana vyuo, vijana wa kidato cha sita walio katika mitihani yao nao warudi shuleni kuanzia Juni 1 na wizara ipange mpango mzuri ili wanafunzi wafanye mitihani yao bila kuathiri mpango wa kwenda Chuo Kikuu“ JPM. Kwa maelezo zaidi na kuona video bofya link hapo chini.
https://millardayo.com/jpm-vyuo-vifunguliwe-mwezi-ujao-form-six-warudi-shule-pia-video/
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.