"Mmeaminiwa na Serikali katika kusimamia huu uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024,Hakikisheni Mnatenda haki Kwa kuwa wazalendo na Uaminifu Mkubwa katika Kutekeleza zoezi linalotarajiwa kufanyika Tarehe 27,Novemba 2024".
Kauli hii imetolewa na Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Mbulu Bi.Rehema Bwasi wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Wasimamizi wa Vituo vya Uchaguzi yaliyofanyika Katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Chief Sarwatt.
Ameeleza kuwa kazi hii ya Uchaguzi lazima ifanyike kwa uzalendo na Usahihi Mkubwa huku tukizingatia Sheria,kanuni na taratibu.
Ikumbukwe Ni Siku Nne Zimesalia kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024,Jumla ya Wasimamizi wa Vituo 492 wamepatiwa mafunzo katika Halmashauri ya Mji wa Mbulu ambapo Jumla ya Vituo 246 vitatumika katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa tarehe 27/11/2024.
"Serikali za Mitaa Sauti ya Wananchi,jitokeze kushiriki uchaguzi"
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.