• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Barua pepe kwa wafanyakazi |
Halmashauri ya Mji Mbulu
Halmashauri ya Mji Mbulu

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Mbulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Biashara Viwanda na Uwekezaji
      • Mipango na Uratibu
      • Kilimo Mifugo na Uvuvi
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • UKAGUZI WA NDANI
      • USIMAMIZI WA MANUNUZI
      • FEDHA NA UHASIBU
      • MAWASILIANO SERIKALINI
      • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
      • HUDUMA ZA SHERIA
      • UHIFADHI WA MALIASILI NA MAZINGIRA
      • USIMAMIZI WA TAKA NA USAFI WA MAZINGIRA
  • Machapisho
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Kituo cha Habari
    • Press Release
    • Video
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Matukio
  • Miradi
    • Approved Project
    • Ongoing Project
    • Completed Project
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Huduma kwa watumishi
    • Maij
    • Elimu
    • Uvuvi
  • Kata
    • Ayamaami
    • Ayamohe
    • Bargish
    • Daudi
    • Endagikot
    • Gehandu
    • Gunyoda
    • Imboru
    • Kainam
    • Marangw
    • Murray
    • Nahasey
    • Nambis
    • Sanubaray
    • Silaloda
    • Tlawi
    • Uhuru
  • Uwekezaji
  • Madiwani
    • Peter Martin Sulle - Sanubaray
    • Alexander Amnaay Tango - Gehandu
    • Ally Akonaay Baha - Ayamohe
    • Anthon John Genda - Tlawi
    • Asia Shabani Amnaay - Bargish
    • Augustino Nade Panga - Nahasey
    • Basili Boay Gwawu - Imboru
    • Bayi Agustino Agapius - Endagikot
    • Emanuel Severino Malle - Kainam
    • Emanuel Akonaay Bura - Murray
    • Juliana Deengw Musso - Gunyoda
    • Kastuli John Umbe - Marang
    • Michael Safari Ami - Nambis
    • Mwajuma Athumani Kabuga - Uhuru
    • Peter Evaristi Golis - Daudi
    • Umbu Margwe Mayo - Ayamaami
    • Vita Kalamu Gilaksa - Silaloda
    • Anna Athanasi Hhayuma - Viti Maalum
    • Bernadetha Andrea Tsere - Viti Maalum

Wasimamizi wa huduma za afya nchini watakiwa kusimamia uwajibikaji

Posted on: March 17th, 2019

Naibu Katibu Mkuu Afya, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dkt. Dorothy Gwajima amewagiza waratibu wa timu za usimamizi huduma za afya Mikoa (RHMT) na Halmashauri (CHMT) nchini kuhakikisha, wameimarisha mifumo ya uwajibikaji ili kuleta mabadiliko katika sekta ya afya nchini.

Ameyasema hayo alipokuwa kwenye mwendelezo wa ziara zake za kikazi kwa lengo la kukagua uwajibikaji wa timu hizi kwa Mkoa wa Dodoma katika kituo cha afya cha Bahi kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Jijini Dodoma.

Dkt. Gwajima amesema, zoezi la kuwapima uwajibikaji limeanzia Mkoani Dodoma likiwa ni endelevu ambapo ndani ya siku 90 litakuwa limekamilika nchi nzima ambapo wale wote wasiopenda kubadilika watapangiwa majukumu mengine wanayoyamudu.

“Hakuna haja ya kila siku semina, washa, mikutano halafu ukienda vituoni, mambo ya kawaida kabisa unakuta hayako vizuri wala takwimu hakuna na hakuna maelezo yoyote yenye mashiko kwa nini hali imekuwa hivyo ilivyo” Amesema Dkt. Gwajima.

Dkt. Gwajima amesema, pamoja na kazi nzuri zinazofanywa katika baadhi ya maeneo, yapo masuala ya msingi ambayo, yanahitaji kusimamiwa vizuri zaidi na na   hayahitaji chochote cha ziada zaidi ya uwajibikaji imara wa viongozi waliopewa dhamana.

Dkt. Gwajima amesema, Serikali haitavumilia kuwa na waratibu ambao, hawaleti msukumo katika kuleta mabadiliko ya uwajibikaji na badala yake wamebaki kusafiri na kuhudhuria semina, washa na mikutano ambayo haileti tija katika maeneo yao ya kazi.

“Inasikitisha kuona baadhi ya waratibu wanahudhuria semina, mikutano na warsha mbalimbali lakini hakuna mabadiliko na wengine hukaa ofisini na hata wanapoenda kutembelea vituo hawaoni mapungufu na wakiyaona hawaandai mpangokazi wa kuboresha na wakiandaa mpangokazi hawafanyi ufuatiliaji bali, wanafungia taarifa kwenye makabatikatika utendaji kazi wa sasa” Anafafanua Dkt. Gwajima.

Aidha, amesema waratibu ambao wanashindwa kwenda na kasi ya usimamizi unaotakiwa enzi hizi, wajipime mapema kabla ya kupimwa na tayari mpaka sasa  Dkt. Gwajima amewabadilisha waratibu kadhaa katika ziara zake baada ya kuona hawasimamii wajibu wao wa msingi bali wanajitetea zaidi kuliko kuonesha njia hata pale ambapo, hapahitaji fedha bali uwajibikaji tu.

“Wakati wa kusema bila takwimu umeisha. Kama umeingia kazini lazima useme umefanya nini? Kama ni wateja je, umehudumia wangapi siyo kulalamika tu watumishi hawatoshi, je umehudumia wateteja wengi kiasi gani kuzidi uwingi wa majukumu uliyowekewa kwa vigezo na takwimu? Uchache wa watumishi siyo namba bali ni sambamba na uwingi wa majukumu kwa takwimu zisizotia shaka.” Amesema  Dkt. Gwajima

Dkt. Gwajima ameawaagiza waratibu kufanya usimamizi na ufuatiliaji  kwa weledi mkubwa ambapo kila mmoja atatakiwa kuonyesha ameona nini na mpangokazi ni upi na umefanikisha ufumbuzi wa changamoto ngapi, kama umekwama je, umechukua hatua gani za kuomba msaada.

Kuhusu ushirikishwaji wa wadau Dkt. Gwajima amezielekeza timu hizo kuwa na  Kamati za Afya za Vituo na Bodi za Afya ambazo, ni wawakilishi wa wananchi ziwezeshwe ili, kuimarisha kiungo kati ya kituo na wananchi wanaowakilishwa na Kamati hizi. Bila kiungo hiki muhimu kati ya vituo na wananchi ni dhahiri kuwa, tutakwama kwenda na kasi tunayohitaji.

Ametoa wito kwa timu za afya nchini kujifunza toka timu za Dodoma ambao, kwa kutumia fursa ya kuwa karibu na Wizara wameona kwa vitendo nini kinatakiwa ili, nao waanze mara moja kuimarisha mifumo na kuanza mbio za mabadiliko kabla zoezi la tathmini ya Wizara halijawafikia hivyo RHMT na CHMT zinahitajika kuwa imara ili, kuchochea huduma bora katika vituo vya tiba.

Dkt.Gwajima ameendelea kusisitiza kuwa, ni wakati wa kila aliyepewa dhamana kuvaa koti la uzalendo na kuakisi kwa vitendo mwendo wa Serikali ya awamu ya tano katika kuleta mabadiliko ya uwajibikaji kwa haraka.

Aidha, amewapongeza watumishi wote ambao, pamoja na changamoto ambazo zipo, wameendelea kupambana na kuleta mabadiliko na amewaasa kutokatishwa tamaa na wachache wasiopenda kubadilika maana, Serikali ina macho na Jamii pia ina macho na inatambua juhudi za kila mmoja na haitawavumilia wale ambao, wanarudisha nyuma kasi ya maendeleo.

Aidha ikumbukwe kuwa  Dkt.Gwajima ameendelea kufanya ziara zake za kikazi za kukagua utendaji kazi wa vituo vya huduma za afya katika  Jiji la Dodoma, Halmashauri ya Wilaya  Chamwino na Halmashauri ya  Wilaya Bahi na itahitimishwa kwa  kuwa na kikao cha Wadau wote ili, kwa pamoja kujionea hali halisi ilivyo na kuwekeana mikataba ya kazi na uwajibikaji.

Matangazo

  • TANGAZO LA HUDUMA ZA KIBINGWA KUANZA KUTOLEWA MBULU MJI May 26, 2025
  • KAMPENI YA UTOAJI WA MATONE YA VITAMINI A NA UPIMAJI WA HALI YA AFYA KWA MTOTO June 01, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA June 02, 2025
  • NJIA YA KUWASILISHA MALALAMIKO KUPITIA eMREJESHO December 16, 2024
  • Ona zote

Habari mpya

  • UMITASHUMTA NA UMISETA KURINDIMA IRINGA 2025

    June 02, 2025
  • WATUMISHI AJIRA MPYA MBULU TC WAPATIWA MAFUNZO YA PSSSF

    May 29, 2025
  • MBULU TC YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI

    May 28, 2025
  • MBULU MJI TUNAJIVUNIA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU-DT REHEMA BWASI

    May 27, 2025
  • Ona zote

Video

HOTUBA YA MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN BUNGENI
More Videos

Tovuti mashuhuri

  • Babati dc Website
  • Hanang' dc Website
  • Babati Town Website
  • Simanjiro Website
  • Kiteto Website
  • Mbuludc Website

Tovuti Mbadala

  • Manyara Reginal Website
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Ikulu
  • BLOG RASMI YA OFISI YA WAZIRI MKUU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali na Majibu
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.