Na Majid Abdulkarim na Mathew Kwembe
Serikaliimewataka watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuimarisha uwezo wa ofisiza Wakaguzi wa ndani ili waweze kusaidia jukumu la usimamizi thabiti wa fedhaza umma.
Agizohilo limetolewa leo na Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa naSerikali za Mitaa bwana Tixon Nzunda katika Chuo cha Serikali cha Serikali zaMitaa Hombolo kilichopo jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa kikao kazi chakupokea na kuhakiki taarifa za majibu na mipango kazi ya utekelezaji wa hoja namapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu zaMamlaka za Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha 2017/2018.
BwanaNzunda amesema kuwa ni wajibu wa Wakurugenzi wa Halmashauri kama MaafisaMasuuli kuhakikisha kuwa wanaimarisha ofisi za wakaguzi wa ndani kwa kuwajengeamazingira mazuri ya kufanya kazi, kuwapa raslimali watu wa kutosha na raslimalifedha.
“Mkaguziwa ndani ni kioo cha taasisi yetu, Mkurugenzi bora hawezi kukosa kuzungumziamisingi ya utawala bora, ambayo ni pamoja na kuhakikisha kuwa anajenga misingithabiti ya usimamizi wa fedha za umma,” amesema bwana Nzunda.
Amesemakwa mujibu wa kifungu cha sheria ya fedha za Serikali za Mitaa Na.9 ya mwaka1982 pamoja na marekebisho yake, Waziri mwenye dhamana ya serikali za Mitaaamepewa wajibu wa kuhakikisha Mamlaka za Serikali za Mitaa zinakuwa nausimamizi thabiti wa fedha.
BwanaNzunda ameongeza kuwa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikalizimekuwa zikibainisha kuwa bado kuna tatizo kubwa la halmashauri kutotekelezamapendekezo ya ukaguzi hasa kwa miaka ya nyuma.
“Taarifaya CAG kwa mwaka 2016/17 ilibainisha kati ya mapendekezo 12,703 yaliyotolewamwaka 2015/16 ni mapendekezo 4,262 sawa na asilimia 34 tu ndiyo yaliyotekelezwakwa ukamilifu,” amesema.
Vilevile bwana Nzunda amesema kati ya maagizo 748 yaliyotolewa na kamati ya LAAC,maagizo yaliyotekelezwa na kukamilika yalikuwa 233 sawa na 31 tu.
Awaliakimkaribisha Kaimu Katibu Mkuu kufungua kikao hicho, Mkurugenzi wa Kitengo chaUkaguzi na Ufuatiliaji wa fedha za Mamlaka za Serikali za Mitaa Bi MiriamMmbaga amesema kuwa kikao hicho kitafanyika kuanzia tarehe 19-26 Machi, 2019ambapo kitawahusisha Wakurugenzi, Waweka Hazina na Wakaguzi wa Ndani kutokaMikoa 26 na Halmashauri zote 185 nchini.
Amesemalengo la kikao hicho ni kuwawezesha Watendaji hao kujibu hoja za CAG, kuongezauwajibikaji katika utendaji wao wa kazi ili hoja hizo zisijitokeze tena katikahalmashauri zao.
Kwamujibu wa Bi Mmbaga takwimu za taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu zaSerikali inaonyesha kuwa katika mwaka wa fedha 2013/14 kati ya hoja 7921zilizoibuliwa ni hoja 2330 sawa na asilimia 29 ndizo zilizopatiwa majibu.
Kufuatiakuibuliwa kwa hoja hizo za CAG, Ofisi ya Rais TAMISEMI baada ya kupokea maagizoya Waziri Mkuu iliwataka Wakuu wa Mikoa wasimamie na kujadili utekelezaji wamapendekezo ya CAG na kuchukua hatua ambapo jumla ya watumishi 203 kutokaMamlaka za Serikali za Mitaa walichukuliwa hatua za kinidhamu na za kisheria.
Kwaupande wake Mkaguzi wa ndani Mkuu wa Serikali Msaidizi anayeshughulikiaSerikali za Mitaa bwana Mwanyika Semroki amesema kuwa ni vyema watendaji waMamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha kuwa wanazingatia udhibiti nausimamizi imara wa fedha za umma hasa kwa kutambua maeneo au miradi iliyokwenye hatari ya kufanyiwa ubadhilifu.
Ujenzi
Anuani: P.O Box 164 Mbulu
Simu: +255 272 2533331
Simu ya kiganjani:
Barua pepe: td@mbulutc.go.tz
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.