• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Barua pepe kwa wafanyakazi |
Halmashauri ya Mji Mbulu
Halmashauri ya Mji Mbulu

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Mbulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Biashara Viwanda na Uwekezaji
      • Mipango na Uratibu
      • Kilimo Mifugo na Uvuvi
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • UKAGUZI WA NDANI
      • USIMAMIZI WA MANUNUZI
      • FEDHA NA UHASIBU
      • MAWASILIANO SERIKALINI
      • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
      • HUDUMA ZA SHERIA
      • UHIFADHI WA MALIASILI NA MAZINGIRA
      • USIMAMIZI WA TAKA NA USAFI WA MAZINGIRA
  • Machapisho
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Kituo cha Habari
    • Press Release
    • Video
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Matukio
  • Miradi
    • Approved Project
    • Ongoing Project
    • Completed Project
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Huduma kwa watumishi
    • Maij
    • Elimu
    • Uvuvi
  • Kata
    • Ayamaami
    • Ayamohe
    • Bargish
    • Daudi
    • Endagikot
    • Gehandu
    • Gunyoda
    • Imboru
    • Kainam
    • Marangw
    • Murray
    • Nahasey
    • Nambis
    • Sanubaray
    • Silaloda
    • Tlawi
    • Uhuru
  • Uwekezaji
  • Madiwani
    • Peter Martin Sulle - Sanubaray
    • Alexander Amnaay Tango - Gehandu
    • Ally Akonaay Baha - Ayamohe
    • Anthon John Genda - Tlawi
    • Asia Shabani Amnaay - Bargish
    • Augustino Nade Panga - Nahasey
    • Basili Boay Gwawu - Imboru
    • Bayi Agustino Agapius - Endagikot
    • Emanuel Severino Malle - Kainam
    • Emanuel Akonaay Bura - Murray
    • Juliana Deengw Musso - Gunyoda
    • Kastuli John Umbe - Marang
    • Michael Safari Ami - Nambis
    • Mwajuma Athumani Kabuga - Uhuru
    • Peter Evaristi Golis - Daudi
    • Umbu Margwe Mayo - Ayamaami
    • Vita Kalamu Gilaksa - Silaloda
    • Anna Athanasi Hhayuma - Viti Maalum
    • Bernadetha Andrea Tsere - Viti Maalum

Baraza La Madiwani la Halmashauri ya Mji wa Mbulu lajadili na kupitisha Makisio ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2021/2022 Kiasi cha Shilingi Bilioni 20.8 – Wito watolewa kasi ya ukusanyaji wa mapato ya ndani

Posted on: February 27th, 2021

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji wa Mbulu limepitisha Bajeti ya Halmashauri hiyo yenye thamani ya Shilingi Bilioni 20.8 kwa mwaka wa fedha 2021/2022, kutoka vyanzo mbalimbali ambavyo ni Ruzuku ya Serikali Kuu, Wahisani na Wadau wa maendeleo, Mapato ya ndani na Michango ya wananchi.

Kikao maalum cha Baraza la Madiwani kimefanyika tarehe 26 Februari 2021 na tarehe 27 Februari 2021 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu (Ukumbi wa Maendeleo ya Jamii) ambapo Waheshimiwa Madiwani wameiomba Halmashauri kupitia mapato yake ya ndani ihakikishe kuwa kila Kata inapata kiasi cha Shilingi Milioni 20 ili kurudisha imani kwa Wananchi wao  kutokana na namna wanavyojitolea katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Katika kikoa hicho maalumu, Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe. Chelestino Mofuga alianza kwa kuwakumbusha waheshimiwa madiwani kuwa Baraza la Madiwani ni chombo mahususi cha kisheria na ni Bunge la Halmashauri kwa misingi hiyo chombo hicho kinapaswa kuendeshwa kwa misingi ya kisheria na kanuni ambazo zimewekwa.

Aliwaasa waheshimiwa madiwani kufanya kazi kwa kushirikiana na wataalamu wa Halmashauri ili kuleta maendeleo kwa wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu.

Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Mhe. Chelestino Mofuga akifafanua jambo wakati wa kikao maalum cha Baraza la Madiwani kujadili Mpango wa Maendeleo na Bajeti ya Halmashauri ya Mji wa Mbulu  kwa mwaka fedha 2021/2022 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri tarehe
26 Februari 2021.

Awali akiwasilisha Mpango wa Maendeleo na Bajeti ya Halmashauri ya Mji wa Mbulu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu Mama Anna P. Mbogo,  amesema bajeti hiyo imezingatia mambo yote muhimu ikiwemo Dira ya Taifa ya Maendeleo, Mpango wa Tatu wa Maendeleo ya Taifa, Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 – 2025, Sheria ya Bajeti pamoja na maendeleo endelevu.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mwaka wa fedha 2021/2022 Halmashauri ya Mji wa Mbulu inalenga kukusanya na kutumia Tshs. 20,856,323,542/= kutoka katika vyanzo mbalimbali.” Alisema Mkurugenzi.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu aliendelea kufafanua kuwa mapato ya ndani ni Tshs. 1,405,510,904/=, Fedha za  Ruzuku ya Mishahara Tshs. 15,217,062,000/=, Fedha za Ruzuku ya Matumizi mengineyo ni Tshs. 863,276,000/=, Fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo Tshs. 2,589,974,638/=, na michango wa wanachi Tshs. 780,500,000/=.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu Mama Anna P. Mbogo akiwasilisha Mpango wa Maendeleo na Bajeti ya Halmashauri ya Mji wa Mbulu kwa mwaka fedha 2021/2022 katika kikao maalum cha Baraza la Madiwani kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri tarehe 26 Februari 2021.

Akizungumza wakati wa kufunga kikao hicho Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu, Mhe. Peter Martin Sulle amewasisitiza wajumbe kuhakikisha kuwa wao kama viongozi wanasimamia vizuri mapato ya Halmashauri. Mhe. Peter Martin Sulle aliwaasa na kuwaomba Wakuu wa Idara na Vitengo kufanya kazi kwa ushirikiano wa pamoja na waheshimiwa Madiwani ili kufanikisha malengo waliyojiwekea kuhakikisha Halmashauri ya Mji wa Mbulu inaendelea kukua kiuchumi.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu, Mhe. Peter Martin Sulle wakati wa akifungua kikao maalum cha Baraza la Madiwani kilichoketi kujadili Mpango wa Maendeleo na Bajeti ya Halmashauri ya Mji wa Mbulu kwa mwaka fedha 2021/2022 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri tarehe 26 Februari 2021.

 

Mbunge wa Jimbo la Mbulu Mjini Mhe. Isaay Zakaria Paulo akichangia hoja wakati wa kikao maalum cha Baraza la Madiwani kilichoketi kujadili Mpango wa Maendeleo na Bajeti ya Halmashauri ya Mji wa Mbulu kwa mwaka fedha 2021/2022 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri tarehe 26 Februari 2021.

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya  Mji wa Mbulu Mhe. Alexender A. Tango akichangia hoja wakati wa kikao maalum cha Baraza la Madiwani kilichoketi kujadili Mpango wa Maendeleo na Bajeti ya Halmashauri ya Mji wa Mbulu kwa mwaka fedha 2021/2022 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri tarehe 26 Februari 2021.


Baadhi ya Waheshimiwa Madiwani wakichangia hoja wakati wa kikao maalum cha Baraza la Madiwani kilichoketi kujadili Mpango wa Maendeleo na Bajeti ya Halmashauri ya Mji wa Mbulu kwa mwaka fedha 2021/2022 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri tarehe
26 Februari 2021.

 Baadhi ya Waheshimiwa Madiwani  wakifuatilia wasilisho la Mpango wa Maendeleo na Bajeti ya Halmashauri ya Mji wa Mbulu  kwa mwaka fedha 2021/2022 wakati wa kikao maalum cha Baraza la Madiwani kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri tarehe
26 Februari 2021. 

Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu Bwana. Edward Mboya akijibu baadhi ya hoja zinazohusu masuala ya Utumishi wakati wa kikao maalum cha Baraza la Madiwani kilichoketi kujadili Mpango wa Maendeleo na Bajeti ya Halmashauri ya Bahi kwa mwaka fedha 2021/2022 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri tarehe 26 Februari 2021.

Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya yaMbului, wakifuatilia wasilisho la Mpango wa Maendeleo na Bajeti ya Halmashauri ya Mji wa Mbulu  kwa mwaka fedha 2021/2022 wakati wa kikao maalum cha Baraza la Madiwani kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri tarehe 26 Februari 2021.


Matangazo

  • TANGAZO LA HUDUMA ZA KIBINGWA KUANZA KUTOLEWA MBULU MJI May 26, 2025
  • KAMPENI YA UTOAJI WA MATONE YA VITAMINI A NA UPIMAJI WA HALI YA AFYA KWA MTOTO June 01, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA MJI WA MBULU June 09, 2025
  • NJIA YA KUWASILISHA MALALAMIKO KUPITIA eMREJESHO December 16, 2024
  • Ona zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA NGAZI ZOTE MBULU TC WAMAETAKIWA KUSHIRIKIANA KATIKA UTOAJI WA TAARIFA ZA VITENDO VYA UKATILI

    June 30, 2025
  • MHE.SEMINDU AONGOZA KIKAO CHA MAANDALIZI YA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2025.

    June 26, 2025
  • WATUMISHI MBULU TC WAKUMBUSHWA UMUHIMU WA MATUMIZI YA E-UTENDAJI.

    June 23, 2025
  • TUZO YA PONGEZI MBULU TC

    June 20, 2025
  • Ona zote

Video

HOTUBA YA MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN BUNGENI
More Videos

Tovuti mashuhuri

  • Babati dc Website
  • Hanang' dc Website
  • Babati Town Website
  • Simanjiro Website
  • Kiteto Website
  • Mbuludc Website

Tovuti Mbadala

  • Manyara Reginal Website
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Ikulu
  • BLOG RASMI YA OFISI YA WAZIRI MKUU
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali na Majibu
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.